ZSSF YAZINDUA MAEGESHO YA MAGARI MICHENZANI MALL
 Katika shamrashamra za kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964 Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF umefungua maegesho ya magari katika eneo la Michenzani Mall.


Akisoma hutba yake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita  amesema ni wajibu wa kila mwananchi kuyatumia vyema maeneo hayo Ili kuendelea kuwa na haiba nzuri.

Aidha Mh. Tabia amezitaka tasisi zote zinazoshuhulikia usalama barabarani na Mipango miji kuchukua hatua stahiki Kwa magari na vyombo vya moto ambavyo vinaegeshwa maeneo yasiyo rasmin Kwa kupewa adhalikali  ili kuondoa msongamano wa vyombo .


Sambmba na hayo amewashajihisha wafanyabishara kujiunga na Mfuko wa hiyari wa ZVSSS Ili kuchangia katika miradi ya maendeleo na kujiwekea hakiba ya baadae.


Kwaupande wake Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Bw. Nassor Shaabani Ameir amesema mradi huo ni mwanzo wa miradi mingine mingi ya maegesho ya magari ya kisasa inayofanywa na Mfuko huo.


Akitoa maelezo ya ujenzi huo Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Bw. Rashid Saidi Rashid amesma mradi huo utasaidia kuondoa usumbufu Kwa wananchi wanaotaka kuegesha vyombo vyao, Pia amesema mradi huo umegharimu zaidi ya silingi milioni 86 hadi kukamilika kwake.

Mradi huo wa maegesho ya magari ambao umezinduliwa umeanza rasmin tarehe 27 April 2022 na kufunguliwa leo January  4, 2023  ambapo umejumuisha maegesho ya magari 79, sehemu 6 za ATM, choo kimoja, mfumo wa kuruhusu kuingia na kutoka magari Control Room  moja, maeneo ya kuegeshea vyombo vya maringi mawili 16 na CCTV camera 6 .